Wednesday 28 October 2015

Sikukosa Kungojea

[Kiswahili Kitukuzwe] Kroxti:


Yamkini, sikukosea kungojea. Sikujitilia doa kuungoja wakati wangu. Na ulipowadia, sikungoja kuukosa. Nilipita nao. Nilifunua mabawa nikapaza sauti kisha nikapaa angani. Mwenye sikio na aniskize. Mawingu yasiyo kasoro yaliniamkua yakitaka kujua nilivyokuja kukua. Wakaniuliza nilivyokuwa. Dakika za kuomboleza zimenipiga chenga na kwa uhakika, nilizobaki nazo kwa sasa ni dakika za furaha. Asiyejua furaha hapati furaha. Mpaka lini tena nitasahau nilipotoka? Mpaka lini tena nitakumbuka mara nilizoanguka? Sikuchoka na sitachoka. Japo baridi lanilaza, sitatetemeka. Sitaogopa tena. Ni muda wangu huu na sitababaika. Akufuzaye wakati mwingine hukuambia toka. Na lisilokulisha lisikutishe. Chakula kingi ufukoni. Ya pesa tayarisha mfukoni. Dawa ya uoga si fujo. Ni kunyenyekea na kujifunza kukwaa hata juu zaidi, zaidi ya shida zako. Hatukosei tunapotaka; tunakosea tunapotaka kwa nia mbaya. Jizungumzie na ujipende ulivyo. Tazama mbali zaidi na usiogope kutenda. Lako likifika; lako utalipata. 

No comments:

Post a Comment